top of page
Search
  • Writer: Rukhsana Noor
    Rukhsana Noor
  • Jul 5, 2020
  • 1 min read


Mahitaji:


Samaki wawili

Chumvi

Limao au ndimu moja

Kitunguu saumu kilichopondwa nusu kijiko cha chakula

Mafuta ya kupikia

Pilipili manga kijiko kimoja cha chakula

Tangawizi iliyopondwa nusu kijiko cha chakula

Binzari ya mchuzi nusu kijiko cha chakula

Kitunguu maji

Hoho

Carrot

Nyanya

Karanga iliyosagwa kijiko kimoja cha chakula


Jinsi ya kupika:


1) Tengeneza samaki wako osha kisha wawekee ndimu au limao, chumvi na pilipili manga nusu kijiko waache kwa dk 30 kisha wakaange uweke pembeni


2) Weka sufuria jikoni, kisha weka mafuta vijiko vitatu vya chakula yakipata moto weka kitunguu maji na carrot kaanga,vikipata rangi weka kitunguu saumu, pilipili manga iliyobaki,binzari ya mchuzi,tangawizi kisha kaanga, kisha weka nyanya na chumvi kidogo funika acha nyanya iive , nyanya ikiiva weka hoho koroga na uweke karanga weka na maji nusu kikombe changanya kisha funika tena mchuzi uchemke, ukisha chemka ukawa mzito weka samaki wako changanya na uache uchemke dk 2 kisha epua utakuwa tayari.

 
 
 

© 2020 by Roxy recipes. All rights reserved

  • ooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooroxyrecipes Instagram Account
bottom of page