- Rukhsana Noor
- Aug 27, 2020
- 1 min read
Mahitaji:
Ukwaju kiasi utakachopenda (nimetumia mitano)
Chumvi
Binzari nyembamba ya unga/binzari ya pilau kijiko kimoja cha chai
Pilipili iliyosagwa au kupondwa kijiko cha chai (si lazima)
Kitunguu saumu na tangawizi zilizopondwa kijiko kimoja cha chakula
Mafuta ya kupikia kijiko kimoja cha chakula
Masala ya mchuzi kijiko kimoja cha chakula
Jinsi ya kutengeneza:
1) Osha ukwaju na maji safi kisha weka maji kiasi na uchemshe, kisha uchuje utoe kokwa upate rojo na uweke pembeni rojo yako
2) Chukuwa pan weka jikoni, weka mafuta ya kupikia, kisha weka masala ya mchuzi, kitunguu saumu na tangawizi, binzari nyembamba, pilipili kaanga kwa sekunde 10, kisha mimina rojo ya ukwaju uweke na chumvi na anza kuipika huku unaikoroga mpaka iwe nzito kwa uzito unaotaka wewe kisha epua itakuwa tayari, ni nzuri kula na chips, mishkaki n.k