top of page
Search

Maandazi ya nazi

  • Writer: Rukhsana Noor
    Rukhsana Noor
  • Jul 4, 2020
  • 1 min read


MAHITAJI:


unga wa ngano vikombe viwili (500ml)

Tui la Nazi kikombe kimoja (250ml)

Sukari kikombe kimoja (250ml)

Amira ya chenga 2tbsp

Banking powder 1tsp (mimi hutumia chapa mandashi)

Hiliki ya unga 1tbsp

Chumvi 1/2 tsp

Mafuta ya kupikia


JINSI YA KUPIKA:


1) Chukuwa unga weka katika bakuli pana kisha weka sukari,chumvi, hiliki, mafuta ya kula kijiko kimoja, banking powder changanya weka pembeni , pasha tui liwe vuguvugu chota vijiko vitatu weka katika bakuli dogo weka amira changanya na tui funika iumuke, ikishaumuka mimina katika bakuli la unga changanya kisha tumia tui kukanda unga, kanda mpaka ulainike kisha pakaa donge lako mafuta funika kwa masaa mawili liumuke


2) Likisha umuka kata madonge ya size unayotaka ya mandazi kisha funika tena madonge yaumuke, yakiumuka sukuma donge moja usifanye nene wala jembamba ukisha sukuma kama chapati kata vipande vinne vya mandazi kisha fanya hivyo mpaka madonge yaishe na funika tena mandazi yaumuke yakisha umuka weka karai jikoni tumia moto mdogo mafuta yakipata moto kiasi anza kuchoma mandazi yako mpaka yaishe.

 
 
 

Recent Posts

See All

Comentarios


© 2020 by Roxy recipes. All rights reserved

  • ooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooroxyrecipes Instagram Account
bottom of page