top of page
Search

NYAMA YA KUKAANGA

  • Writer: Rukhsana Noor
    Rukhsana Noor
  • Mar 24, 2020
  • 1 min read

Updated: Mar 27, 2020




MAHITAJI:

Nyama ya Ng`ombe steki nusu kilo

chumvi

mafuta ya kupikia

tangawizi na kitunguu saumu kilichopondwa vijiko viwili vya chakula

soy sauce vijiko vitatu

vinegar kijiko kimoja

pilipili manga ya unga nusu kijiko


JINSI YA KUPIKA:


1) Osha na katakata nyama na uweke katika bakuli pana

2) Weka vitu vyote kasoro mafuta,katika bakuli lenye nyama na uchanganyaje vizuri ukimaliza ifunike ka muda wa masaa matatu

3) Baada ya masaa matatu weka mafuta katika pan tumia moto mdogo mdogo yakipata moto weka nyama zote funika, acha zijipike kwa moto mdogo kwa dakika 40 kisha zigeuze funika tena acha zijipike tena kwa dk 40 kisha geuza fanya hivyo mpaka nyama zako ziive ziwe za brown kisha zitoe katika mafuta tayari kwa kuliwa na ugali au kitu chochote.




























 
 
 

Recent Posts

See All

Comments


© 2020 by Roxy recipes. All rights reserved

  • ooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooroxyrecipes Instagram Account
bottom of page