top of page
Search

Rolls za Mdalasini

  • Writer: Rukhsana Noor
    Rukhsana Noor
  • May 12, 2020
  • 1 min read


MAHITAJI:

Unga wa ngano vikombe vitano (tumia 250ml cup)

Siagi iliyoyeyushwa vijiko vikubwa vya chakula viwili

Siagi usiyoyeyusha vijiko vitatu vikubwa vya chakula

Maziwa ya maji nusu lita

Mdalasini wa unga vijiko vitatu vya na nusu vya chakula

Sukari ya brown vijiko vitatu vikubwa

Sukari nyeupe vijiko vitatu vya chakula

Hamira ya chenga kijiko kimoja kikubwa na nusu

Yai moja

Banking powder kijiko kimoja kidogo


JINSI YA KUTENGENEZA:


1) chukuwa bakuli pana weka unga, banking powder na sukari nyeupe changanya weka pembeni


2) Chukuwa bakuli lingine weka sukari ya brown na mdalasini changanya kisha weka pembeni


3) Chukuwa bakuli lingine weka siagi yote iliyoyeyushwa, maziwa, yai na amira ya chenga changanya mpaka amira iyeyuke na ipande juu


4) Kisha tumia mchanganyiko wa maziwa, amira,yai na siagi kuukandia unga kanda unga uwe laini utaona unaganda mikononi ni sawa unaweza pakaa mafuta katika mikono ili usikunatie ukimaliza kukanda unga uweke katika bakuli kubwa lipakae mafuta ili usinatie kisha funika kwa lisaa limoja uumuke


5) ukisha umuka kata madonge ya size kiasi usukume kama chapati donge moja moja


6) Ukisha sukuma donge la kwanza chukuwa siagi isiyoyeyushwa pakaa juu ya hilo donge ulilosukuma hakikisha umepakaa kote kisha chukuwa mchanganyiko wa mdalasini na sukari anza kunyunyizia Juu ukimaliza roll hilo donge lako kisha chukuwa kisu anza kukata madonge unayotaka, fanya hivyo mpaka madonge yako yaishe


7) Chukuwa pan la oven la kuokea pakaa mafuta kisha panga rolls zako acha nafasi kati ya roll moja na nyingine ili ukiumua tena zipate nafasi kisha funika acha tena yaumuke kwa dk 30 yakisha umuka oka katika moto wa 180C kwa dk 25 baada ya hapo toa zitakuwa tayari. Enjoy

 
 
 

Recent Posts

See All

Comments


© 2020 by Roxy recipes. All rights reserved

  • ooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooroxyrecipes Instagram Account
bottom of page