Tips za kupika chapati za kusukuma laini
- Rukhsana Noor
- Mar 24, 2020
- 1 min read
Updated: Mar 27, 2020
Kwanini upike chapati za kusukuma ngumu, Hizi hapa ni tips za kufuata.....
Hakikisha unakanda unga unalainika
Wakati wa kukanda hakikisha unakadiria maji saa na unga usiutepeteshe unga kisha ukaongeza unga mbichi juu kuufanya ushikane ili uendelee kukanda kufanya hivi kutafanya unga kuwa mgumu
Ukisha kanda unga kuwa unaufunika kwa saa moja kabla ya kukunja chapati
Ukisha kunja chapati hakikisha muda wote umezifunka wakati unapika , zingine usiziache wazi zinazosubiria kupikwa
Wakati wa kupika usipike na kikaango kikavu kipate mafuta kidogo kila mara unapotaka kuweka chapatti
Tumia moto wa kati kupikia chapati usiwe mkali wala mdogo sana
Unapoweka chapati katika kikaango baada ya kupata rangi upande mmoja unapoigeuza ipate rangi upande wa pili iache uone inavimba ndio uweke mafuta
Commentaires