Vanilla Cake
- Rukhsana Noor
- May 12, 2020
- 1 min read

Vanilla cake
MAHITAJI:
unga wa ngano gram 560
Mayai 6
Sukari nusu kilo
Vanilla sugar kijiko kimoja au vanilla ya maji vijiko viwili
Chumvi kijiko kimoja kidogo
Banking soda kijiko kimoja kidogo
Blue band gram 350
Maziwa 310ml
JINSI YA KUPIKA:
1) Weka sukari yote na siagi yote katika bakuli pana na utumie hand mixer kumix mpaka vilainike kavisa viwe laini
2) Kisha weka yai moja moja huku ukiendelea kusaga mpaka yasagike yote na yachanganyike vizuri
3) Kisha anza kuweka maziwa kidogo kidogo huku ukiendeea kumix kisha weka vanilla endelea kumix
4) Kisha anza kuweka unga kidogo kidogo huku unachanganya unaweza tumia mwiko kuchanganyia unga hand mixer haina haja tena ukimaliza andaa kifaa chako cha kuokea kipake mafuta au siagi kisha mimina mcganganyiko wako na uoke keki yako kwa dk45 kwa moto wa 150c, baada ya hapo itakuwa tayari. Enjoy 😋
Comments