top of page
Search
  • Writer: Rukhsana Noor
    Rukhsana Noor
  • Jul 11, 2020
  • 1 min read

Mahitaji:

Kunde za kupaaza vikombe viwili

Vitunguu maji viwili

Kotmir (majani ya giligilani) kiasi utakachopenda

Chumvi

Vitunguu saumu punje sita

Pilipili manga 1 tsp (kijiko cha chai)

Binzari nyembamba 1 tsp

Mafuta ya kupikia


Jinsi ya Kupika:


1) Chagua na roweka kunde kwa masaa sita au usiku kucha, kisha zioshe na uzitoe maganda


2) Ziweke katika jagi la blender, kisha weka na kitunguu maji kilichokatwakatwa, punje za vitunguu saumu, binzari nyembamba na maji kidogo saga zilainike kisha weka katika chujio zichuje maji


3) Zikishachuja maji weka chumvi, pilipili manga na ukatie katie majani ya giligilani uchanganye


4) Weka karai la mafuta jikoni tumia moto wa kiasi ili ziive na ndani ukiwa mkali sana zitaiva nje ndani bado, mafuta yakipata moto choma bagia zako baada ya hapo zitakuwa tayari.

 
 
 
  • Writer: Rukhsana Noor
    Rukhsana Noor
  • Jul 7, 2020
  • 1 min read

Mahitaji:

Vipande vya kuku unavyotaka

Hoho moja

Carrot moja

Vitunguu maji vitatu

Chumvi

Limao au ndimu moja

Tangawizi iliyopondwa 1/2 tbsp (kijiko cha chakula)

Pilipili manga ya unga 1tsp (kijiko cha chai)


Jinsi ya kupika:


1) Osha vipande vya kuku weka katika sufuria weka chumvi na kamulia ndimu au limao kisha bandika jikoni ichemke iive na ibaki na maji ya kutosha kwa supu kisha epua


2) Toa vipande vya kuku katika supu uliyochemshia weka pembeni, kisha Katakata vitunguu, hoho na carrots weka katika supu uliyochemshia kuku, weka na tangawizi na pilipili manga rudisha jikoni chemsha viive kisha epua ipoe


3) Ikishapoa mimina katika jagi la blender kisha saga ukimaliza mimina ndani ya sufuria weka na vipande vya kuku rudisha tena jikoni kwa dk 2 ichemke kisha epua itakuwa tayari.


 
 
 

© 2020 by Roxy recipes. All rights reserved

  • ooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooroxyrecipes Instagram Account
bottom of page