top of page
Search
  • Writer: Rukhsana Noor
    Rukhsana Noor
  • Jul 22, 2020
  • 1 min read


Mahitaji:


Unga wa ngano vikombe vinne (kikombe kimoja cha 250ml)


Maziwa ya maji vikombe viwili ( 500ml)


Siagi vijiko viwili vya chakula (yeyusha)


Siagi vijiko vitatu vya chakula (usiyeyushe)


Amira ya chenga vijiko viwili vya chakula


Sukari kikombe kimoja 250ml


Mafuta ya kula kijiko kimoja cha chakula


Jinsi ya kupika:


1) Pasha maziwa yawe vuguvugu kidogo sana kisha weka siagi uloyeyusha, amira ya chenga na mafuta na sukari kidogo koroga kisha acha iumuke amira


2) Chukuwa unga changanya na sukari yote iliyobaki kisha mimina kidogo kidogo katika mchanganyiko wa maziwa na amira kisha kanda unga wako mpaka uchanganyike vizuri uwe Donge kisha tumia vijiko vya siagi visivyoyeyushwa kuwa unapaka katika donge lako huku unakanda mpaka iishe ukimaliza kukanda paka mafuta donge lako funika kwa masaa mawili liumuke


3) Ukishaumuka kata madonge ya sliders zako pakaa mafuta trey ya kuokea uyapange acha nafasi kati ya donge na donge kisha funika kwa dk 45 yaumuke tena kisha yapakae mafuta juu, kisha oka katika moto wa 150c kwa dk45 baada ya hapo zitakuwa tayari.


 
 
 
  • Writer: Rukhsana Noor
    Rukhsana Noor
  • Jul 22, 2020
  • 1 min read


Mahitaji:


Pilipili ndefu kiasi utakachopenda

Mafuta ya kupikia

Nyanya mbili zilizosagwa

Chumvi

Binzari masala kijiko kimoja cha chakula

Binzari ya njano kijiko kimoja cha chai

Kitunguu saumu kilichopondwa kijiko kimoja cha chai

Maji ya limao au ndimu kijiko cha chakula kimoja


Jinsi ya kupika:


1) Osha pilipili zako kisha ziache zikauke maji


2) Weka sufuria jikoni ya mafuta yakipata moto kiasi (yasiwe ya moto sana viungo vitaungua), weka viungo vyote na vikaange kwa sekunde 5, kisha weka nyanya ipike mpaka iive mafuta yaje juu, kisha weka pilipili zote changanya weka chumvi na maji ya limao funika na ipike mpaka pilipili ziive ziwe laini unaweza ongeza maji kidogo ukiona nyanya zinaganda chini. Zikiiva pilipili epua acha ipoe itakuwa tayari kuliwa.

 
 
 
  • Writer: Rukhsana Noor
    Rukhsana Noor
  • Jul 15, 2020
  • 1 min read

Mahitaji:

Mchele vikombe viwili

Chumvi

Mafuta ya kupikia

Vitunguu maji vinne

Majani ya kotmir kiasi utakachopenda


Jinsi ya kupika:

1) Chagua na osha mchele wako uchuje maji uweke pembeni


2) Menya vitunguu na uvikate kwa urefu kisha vikaange viwe brown na uvichuje mafuta uviweke pembeji, osha kotmir na uikatekate


3) Bandika maji ya kupikia wali jikoni weka chumvi yakichemka weka mchele na mafuta upike ukikaribia kukauka maji weka kotmir ugeuze kisha ufunikie ukauke maji uwe tayari


4) Ukishaiva na kukauka maji nyunyizia vitunguu ulivyokaanga na utakuwa tayari kuliwa.

 
 
 

© 2020 by Roxy recipes. All rights reserved

  • ooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooroxyrecipes Instagram Account
bottom of page