top of page
Search
  • Writer: Rukhsana Noor
    Rukhsana Noor
  • Mar 24, 2020
  • 1 min read

Updated: Mar 27, 2020




MAHITAJI:

Nyama ya Ng`ombe steki nusu kilo

chumvi

mafuta ya kupikia

tangawizi na kitunguu saumu kilichopondwa vijiko viwili vya chakula

soy sauce vijiko vitatu

vinegar kijiko kimoja

pilipili manga ya unga nusu kijiko


JINSI YA KUPIKA:


1) Osha na katakata nyama na uweke katika bakuli pana

2) Weka vitu vyote kasoro mafuta,katika bakuli lenye nyama na uchanganyaje vizuri ukimaliza ifunike ka muda wa masaa matatu

3) Baada ya masaa matatu weka mafuta katika pan tumia moto mdogo mdogo yakipata moto weka nyama zote funika, acha zijipike kwa moto mdogo kwa dakika 40 kisha zigeuze funika tena acha zijipike tena kwa dk 40 kisha geuza fanya hivyo mpaka nyama zako ziive ziwe za brown kisha zitoe katika mafuta tayari kwa kuliwa na ugali au kitu chochote.




























 
 
 
  • Writer: Rukhsana Noor
    Rukhsana Noor
  • Mar 24, 2020
  • 1 min read

Updated: Mar 29, 2020





MAHITAJI:

  • Unga wa ngano vikombe viwili

  • Mayai 2

  • Sukari 1/2 kikombe

  • Blue band nusu kikombe

  • Vannila kijiko kimoja

  • Banking powder vijiko vinne vidogo

  • maziwa ya maji nusu kikombe




JINSI YA KUPIKA:


1) Chukuwa bakuli pana weka maziwa,vanilla, sukari mayai na iyeyushe blue band uchanganye , vikisha changanyika chukuwa banking powder weka katika unga changanya kisha anza kuweka unga kidogo kidogo katika mchanganyiko wako mpaka upate mchanganyiko mzito kiasi hapo zitakua tayari kuchoma


2) Andaa chuma chako cha kuchomea waffles ,kisha chota na kijiko mchanganyiko wako weka katika chuma na uanze kupika waffles mpaka unga uishe




 
 
 
  • Writer: Rukhsana Noor
    Rukhsana Noor
  • Mar 24, 2020
  • 1 min read

Updated: Mar 27, 2020

Kwanini upike chapati za kusukuma ngumu, Hizi hapa ni tips za kufuata.....


  1. Hakikisha unakanda unga unalainika

  2. Wakati wa kukanda hakikisha unakadiria maji saa na unga usiutepeteshe unga kisha ukaongeza unga mbichi juu kuufanya ushikane ili uendelee kukanda kufanya hivi kutafanya unga kuwa mgumu

  3. Ukisha kanda unga kuwa unaufunika kwa saa moja kabla ya kukunja chapati

  4. Ukisha kunja chapati hakikisha muda wote umezifunka wakati unapika , zingine usiziache wazi zinazosubiria kupikwa

  5. Wakati wa kupika usipike na kikaango kikavu kipate mafuta kidogo kila mara unapotaka kuweka chapatti

  6. Tumia moto wa kati kupikia chapati usiwe mkali wala mdogo sana

  7. Unapoweka chapati katika kikaango baada ya kupata rangi upande mmoja unapoigeuza ipate rangi upande wa pili iache uone inavimba ndio uweke mafuta

 
 
 

© 2020 by Roxy recipes. All rights reserved

  • ooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooroxyrecipes Instagram Account
bottom of page